Uzima wa Ulimwengu ujao - Mahubiri ya Mch. John Anderson MoshiJUMAPILI, NOVEMBA 26, 2006 ya

 Yohana 5,24-29 

Maneno muhimu: Kutambua thamani ya uhai; uhai Yesu anautaka kwa watu wote; mtu akiipenda nafsi yake, ataipoteza; ...
Waachane na tamaa za kimwili ambazo zaweza kuharibu mwili na nafsi zao....; Yesu akisema wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, watakuwa hai...;  imani ya kiafrika..; si lazima tufikie hatua ya kubishana na Yesu kama wayahudi; swala kubwa hapa ni wapi tunakokwenda hasa...

 

*****************

Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Matayo 16,21-23: Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi kutoka kwa wazee, makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na siku ya tatu atafufuliwa.

Petro akamchukua kando akaanza kumkemea akamwambia, “Mungu apishie hayo mbali! Jambo hili halitakupata kamwe!” 

Lakini Yesu akageuka akamwambia Petro , “Toka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo hayo si ya Mungu bali ya binadamu.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Konrad Raiser

******

Mahubiri ya Luka 2,41-52: ...Kila mwaka wazazi wake walikwenda Yerusalemu kushiriki katika siku kuu ya Pasaka. Yesu alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama desturi ilivyokuwa. Sikukuu ilipokwisha walianza safari ya kurudi nyumbani. Yesu akabaki Yerusalemu pasipo wazazi wake kujua. Wao walidhani yupo nao kwenye msafara kwa hiyo wakaenda mwendo wa siku nzima. Walipotambua kwamba hawakuwa naye, walianza kumtafuta kati ya jamaa na marafiki. Hawakumpata, kwa hiyo wakarudi Yerusalemu wakimtafuta.Siku ya tatu wakamkuta Hek aluni ameketi kati ya walimu wa sheria, akiwasikiliza na kuwau liza maswali. Wote waliomsikia walistaajabishwa na uwezo wake mkubwa wa kuelewa na majibu aliyoyatoa.

Wazazi wake walipomwona walishangaa. Mama yake akamwul iza: “Mwanangu, mbona umetufanyia hivi? Baba yako na mimi tume hangaika kukutafuta kila mahali kwa wasiwasi mkubwa.”

Lakini yeye akajibu: “Kwa nini mlihangaika kunitafuta? Hamkujua ninge kuwa hapa Hekaluni kwenye nyumba ya Baba yangu?" Lakini wao hawakuelewa maana ya jibu lake.

 Akarudi pamoja na wazazi wake hadi Nazareti. Akawa aki watii, na mama yake akayaweka moyoni mambo haya yote. 52 Basi Yesu akaendelea kuongezeka katika kimo na hekima, akipendwa na

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Hans-Dieter Wille

******

Mahubiri ya Luka 3,15.16.21-22:   Siku hizo watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wakijiuliza mioyoni mwao kama Yohana ndiye Kristo. Yohana aliwajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini anayekuja ni mkuu kuliko mimi, sistahili hata kuwa mtumwa wake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto..."....
Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye alibatizwa. Na alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. Roho Mtakatifu akash uka juu yake kama hua; na sauti ikasikika kutoka mbinguni ikisema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa, ninapendezwa nawe.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani  ya Joaquim Nunes

*******

Mahubiri ya Luka 4,14-22: Kisha Yesu akarudi Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu. Habari zake zikaenea katika sehemu zote za wilaya ile.  Alifundisha katika masinagogi yao na wote wakamsifu. Baadaye Yesu akaenda Nazareti, mahali alipokulia. Siku ya sabato alikwenda katika sinagogi kama kawaida yake. Akasimama ili asome Maandiko. Akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifun gua mahali palipoandikwa:  “Roho wa Bwana yu juu yangu. Amenichagua kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatan gazia wafungwa kuwa wako huru, kuwaambia vipofu kuwa wanaweza kuona tena; na kuwaweka huru wanaoonewa, na nitangaze mwaka ambao Bwana atawabariki watu wake.” 

Akakifunga kitabu, akamrud ishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Ndipo akasema: “Maandiko haya mliyosikia nikisoma, leo yametimia.”

Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake mazuri, wakaulizana, “Je, huyu si yule mtoto wa Yusufu?”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Dr. Jürgen Kaiser

*******

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.