Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Marko 12, 28-34: Mwalimu mmoja wa sheria aliwasikiliza wakijadiliana. Alipoona kwamba Yesu amewajibu vizuri, naye akamwuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?”

Yesu akamjibu, “Iliyo kuu ni hii, ‘Sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu ndiye Bwana pekee. Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’ Na sheria ya pili kwa ukuu ndio hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”

Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, ume jibu vyema. Ulivyosema ni kweli kabisa, Mungu ni mmoja wala hakuna mwingine ila yeye. Na kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote; na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka ya kuteketezwa.”

Yesu alipoona jinsi alivyojibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.”

Tangu wakati huo, hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali zaidi.

Hapa kuna mahubiri katika Kiingereza ya Rev. D. Ramón CLAVERÍA Adiego

 

******

Mahubiri ya Yohana 8,3-11: Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya watu wote. Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Katika sheria, Musa ametuamuru kuwapiga mawe wanawake waliokamatwa wakizini, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?”

Walim wuliza hivi kwa kumtega, kusudi wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini akaanza kuandika kwa kidole chake mavumbini. Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Asiyekuwa na dhambi kati yenu awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Akainama tena akaendelea kuandika chini. Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, akianza mkubwa wao. Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama pale walipomwacha. Yesu akasimama akamwuliza, “Mama, wale waliokuwa wanakush taki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?”

Yule mwa namke akajibu, “Hakuna Bwana.”

Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Angelika Volkmann

*******

 

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.