Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Matayo 20,1-16: Yesu:  "Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mtu mwenye shamba la mizabibu aliyeondoka alfajiri kwenda kutafuta vibarua wa kufanya kazi shambani kwake. Wakapatana kuwa atawalipa msha hara wa kutwa, yaani dinari moja, akawapeleka shambani.Mnamo saa tatu akaondoka tena akawakuta watu wengine wamesimama sokoni bila kazi. Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu na nitawalipa haki yenu.’

Kwa hiyo wakaenda. Mnamo saa sita na pia saa tisa alion doka tena akafanya hivyo hivyo. Mnamo saa kumi na moja akaon doka tena akawakuta watu wengine bado wanazurura. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’

Wakamjibu, ‘Ni kwa kuwa hakuna aliyetuajiri.’

Akawaambia, ‘Ninyi pia nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la miza bibu.’

Ilipofika jioni, yule mwenye shamba akamwita msimamizi wa vibarua akamwambia, ‘Waite wafanyakazi uwalipe ujira wao, ukian zia na wale walioajiriwa mwisho na kuishia na wale walioajiriwa kwanza.’

Wale vibarua walioajiriwa mnamo saa kumi na moja, wakaja na kila mmoja wao akalipwa dinari moja. Basi wale wal ioajiriwa kwanza walipofika, walidhani watalipwa zaidi. Lakini kila mmoja wao pia alipewa dinari moja.Walipoipokea, wakaanza kumlalamikia yule mwenye shamba wakisema,  ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu. Ime kuwaje wewe ukawalipa sawa na sisi ambao tumefanya kazi ngumu na kuchomwa na jua mchana kutwa?’

Yule mwenye shamba akamjibu mmoja wao, ‘Rafiki, sija kudhulumu. Je, hatukupatana kwamba utafanya kazi kwa dinari moja? Chukua haki yako uende. Mimi nimeamua kumlipa huyu mtu ali yeajiriwa mwisho sawa na wewe. Je, siwezi kufanya nipendavyo na mali yangu? Au unaona wivu kwa kuwa nimekuwa mkarimu?’

Hali kadhalika, wa mwisho watakuwa wa kwanza na wa kwanza watakuwa wa mwisho.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Katharina Dang

 

******

Mahubiri ya Marko 12,38-44:  Katika mafundisho yake, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi yao rasmi na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa viti vya mbele katika masinagogi na kupewa nafasi za heshi ma katika sherehe. Hao hao ndio huwadhulumu wajane nyumba zao na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Mungu ata waadhibu vikali zaidi.”

Kisha Yesu akaketi karibu na sehemu ya kutolea sadaka Hekaluni akawaangalia watu walivyokuwa wakiweka sadaka zao kwenye chombo cha sadaka. Matajiri wengi waliweka humo kiasi kikubwa cha fedha. Lakini mjane mmoja fukara, alikuja akaweka sarafu mbili zenye thamani ya senti kumi.

Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, “Ninawaambia hakika, huyu mjane ametoa zaidi kuliko wote! Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao; lakini huyu mama ingawa ni fukara, ameweka kila kitu alichokuwa nacho, hata na kile alicho hitaji kwa ajili ya riziki yake.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Eva Tøjner Gøtke

******

Mahubiri ya Luka 16,19-31:  Yesu akasema, “Palikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, alikuwa akiletwa mlangoni kwa huyo tajiri kila siku. Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. Hata mbwa walikuwa wakiramba vidonda vyake.Hatimaye, yule maskini alikufa. Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka, alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake. Akaita, ‘Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.’

Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwa nangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’

Akasema, ‘Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’

Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, ‘Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’

Ibrahimu akamwambia, ‘Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Dr. Jürgen Kaiser

*******

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.