Mahubiri kwa lugha zingine:
Mahubiri ya Matayo 12,38-42: Kisha baadhi ya waandishi wa sheria na Mafarisayo wakam wambia, “Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.”
Lakini yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi. Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu wakati Yona alipowahubiria, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona. Malkia wa Kusini atasimama wakati wa hukumu na kukihukumu kizazi hiki; kwa kuwa yeye alisafiri kutoka miisho ya dunia ili akaisikilize hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.”
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Wolfgang Vögele
Mahubiri ya Marko 15,20-27: Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe. Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe msalaba wa Yesu. Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa. Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa. Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura kuamua kila mtu achukue nini. Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. Tangazo la mashtaka yake liliandikwa maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.” Majambazi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto.
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Cornelia Trick
******
Mahubiri ya Yohana 11,46-52: Lakini wengine walikwenda kwa Mafarisayo wakawaambia mambo Yesu aliyofanya. Kwa hiyo maku hani wakuu na Mafarisayo wakafanya baraza wakaulizana, “Tufa nyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. Kama tukimruhusu aendelee hivi, kila mtu atamwamini; na Warumi watakuja kuharibu Hekalu letu na taifa letu.”
Lakini mmoja wao, aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu kwa mwaka ule akawaambia wen zake, “Ninyi hamjui kitu! Hamwoni kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, badala ya taifa lote kuangamia?”
Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka ule, alikuwa anatabiri kuwa Yesu angekufa kwa ajili ya Wayahudi; na pia kwa ajili ya watoto wa Mungu wal iotawanyika ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja.
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Konrad Raiser
Mahubiri ya Yohana 18,1-19.42: Ndipo Pilato akamtoa Yesu akaamuru apigwe viboko. Askari wakasuka taji ya miiba wakamwekea Yesu kichwani, wakamvika na kanzu ya zambarau. Lakini walipomkaribia Yesu wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu. Kwa hiyo Yesu akatoka nje akiwa amevaa ile taji ya miiba na kanzu ya zambarau. Pilato akawaambia, “Huyu hapa mtu wenu.”
Wale makuhani wakuu na viongozi wa Wayahudi walipomwona wakapiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawajibu, Mchukueni mumsulubishe ninyi, kwa sababu mimi sioni kosa alilo tenda.”
Wao wakamjibu, “Sisi tunayo sheria ambayo inamhukumu kifo kwa sababu yeye anajiita Mwana wa Mungu.”
Pilato aliposi kia haya aliingiwa na hofu. Akaingia ukumbini tena akamwuliza Yesu, “Wewe unatoka wapi?”
Lakini Yesu hakumjibu. Pilato akamwambia, “Kwa nini hunijibu? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachilia huru au kukusulubisha?”
Ndipo Yesu akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka ye yote juu yangu kama Mungu hakukupa mamlaka hayo; kwa hiyo mtu aliyenishtaki kwako ana dhambi kubwa zaidi.”
Tangu wakati huo Pilato akaanza kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakasema, “Ukimwachilia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu ye yote anayejifanya kuwa mfalme anampinga Kaisari.”
Pilato aliposi kia maneno haya alimtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha kuhukumia, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe - kwa Kiebrania paliitwa Gabatha. Siku hiyo ilikuwa ni siku moja kabla ya Pasaka, siku iliyoitwa siku ya Matayarisho, yapata kama saa sita hivi. Pilato Akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa Mfalme wenu!”
Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!”
Pilato akawauliza, “Je, nimsulubishe Mfalme wenu?”
Wale makuhani wakuu wakamjibu, “Hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.”
Ndipo Pilato akawaka bidhi Yesu wamsulubishe. Kwa hiyo wakamchukua Yesu, naye akatoka akiwa amebeba msalaba wake kuelekea mahali palipoitwa, ‘Fuvu la kichwa,’ au kwa Kiebrania, Golgotha. Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubishwa watu wengine wawili, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia wa Yesu. Pilato aliandika maneno yafuatayo kwenye kibao, kikawekwa juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI”.
....Kwa hiyo ili kuka milisha mazishi kabla ya sabato, wakamzika Yesu kwenye hilo kab uri lililokuwa karibu.
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Rev. D. Francesc CATARINEU i Vilageliu
******
Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.