Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Marko 15,16-37: Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika. Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!”

Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.

Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe msalaba wa Yesu. Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa.
Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa. Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura kuamua kila mtu achukue nini.
Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha.Tangazo la mashtaka yake liliandikwa maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.” Majambazi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto.  Na kwa njia hii yale Maandiko yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na wenye hatia,” yalitimia. Watu waliokuwa wakipita, walimtukana na kutikisa vichwa vyao kwa mzaha wakasema, “Si ulikuwa ukisema kwamba unaweza kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? Shuka msalabani basi, ujiokoe mwenyewe!” Hali kadhalika makuhani wakuu na walimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Ali waokoa wengine lakini anashindwa kujiokoa mwenyewe. Kristo mfalme wa Wayahudi ashuke basi msalabani ili tupate kuona na kuamini!”
Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimtukana.

 Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita.  Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”

Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.  Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.

Hapa kuna mahubiri katika  Kijerumani ya Katharina Dang

 

*******

Mahubiri ya Yohnan 6,60-69: Wengi wa wanafunzi wake waliosikia maneno haya walisema, “Mafundisho haya ni magumu! Ni nani awezaye kukubaliana nayo?”

Yesu alitambua kwamba wafuasi wake walikuwa wakilalamika kuhusu mafundisho yake. Kwa hiyo akawauliza, “Mafundisho haya yanawaudhi? Ingekuwaje basi, kama mngeniona mimi Mwana wa Adamu nikirudi mbinguni nilikotoka? Roho wa Mungu ndiye anayetoa uzima, uwezo wa mwanadamu haufai kitu. Maneno haya ni Roho na ni uzima.Lakini baadhi yenu hamuamini.”

Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini na yule ambaye angemsaliti. Akaendelea kusema, “Ndio sababu nili waambia kwamba hakuna awezaye kuja kwangu kama Baba hakumwe zesha.”

Tangu wakati huo wanafunzi wake wengi waliondoka wakaacha kumfuata. Yesu akawauliza wale wanafunzi kumi na wawili, “Ninyi pia mnataka kuondoka?”

Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiye Mtakatifu wa Mungu.”

Hapa kuna mahubiri katika Kiingereza   ya Rev. D. Jordi PASCUAL i Bancells

******

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.