Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Matayo 9,35-37 -10,1.5-10:  Yesu akazunguka kwenye miji yote na vijiji vyote akifundi sha katika masinagogi na kuhubiri Habari Njema za Ufalme, na kuponya kila ugonjwa na kila udhaifu. Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanateseka pasipo msaada, kama kondoo wasio na mchungaji.

Akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini wafa nyakazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno ili awape leke wafanyakazi kwenye mavuno yake.”

 Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka ya kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. ...

Yesu aliwatuma hawa kumi na wawili, akawaagiza, “Msiende kwa watu wa mataifa wala msiingie mji wo wote wa Wasamaria. Bali waendeeni kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia; Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepo kea bure, toeni bure. Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu. Msichukue mikoba ya safari, wala koti la pili, wala viatu, wala fimbo: kwa maana mfanyakazi anastahili riziki yake.

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Angelika Obert

******

Marko 3,31-35: Mama yake Yesu na ndugu zake wakafika wakasimama nje wakamtuma mtu amwite. Umati wa watu waliokuwa wameketi kum zunguka wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wana kutafuta.”

Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?”

Akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka, akasema, “Hawa ndio mama zangu na ndugu zangu. 35 Mtu ye yote anayetenda mapenzi ya Mungu ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya askofu Markus Dröge

******

Luka 14,12-14: Kisha Yesu akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo kar amu ya chakula cha mchana au jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako tajiri; ukifanya hivyo wao nao watakualika kwao na hivyo utakuwa umelipwa kwa kuwaalika. Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu; nawe utapata baraka kwa sababu hawa hawana uwezo wa kukulipa.

Hapa kuna mahubiri katika Kiingereza ya Tim Cain

******

Luka 17,11-19:  Yesu alipokuwa akienda Yerusalemu alipitia kati ya Samaria na Galilaya. Alipokuwa akikaribia kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma walikutana naye. Wakasimama mbali wakaita kwa nguvu, “Yesu! Bwana! tuonee huruma!”  Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Na walipokuwa wakienda, wakapona ukoma wao. Mmoja wao alipoona kwamba ame pona, akarudi kwa Yesu akimsifu Mungu kwa sauti kuu. Kwa heshima kubwa akajitupa miguuni kwa Yesu akamshukuru. Yeye ali kuwa ni Msamaria .

 Yesu akauliza, “Hawakuponywa wote kumi? Wako wapi wale tisa wengine? Hakuna hata mmoja aliyekumbuka kurudi kumsifu Mungu isipokuwa huyu mgeni?”  Akamwambia, “Inuka, uende; imani yako imekuponya.” Ufalme Wa Mungu Utakavyokuja

Hapa kuna mahubiri katika  Kihispania ya P. Conrad J. MARTÍ i Martí OFM

******

Luka 19,1-10:  Yesu akaingia Yeriko, akiwa safarini kuelekea Yerusalemu. Hapo, alikuwapo mtu mmoja mkuu wa watoza kodi na pia mtu tajiri, jina lake Zakayo. Yeye alitamani sana kumwona Yesu lakini hakuweza kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, naye alikuwa mfupi sana. Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu ambaye angepitia njia ile. Yesu alipofika chini ya huo mkuyu, akatazama juu akamwambia: “Zakayo! Shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!”

Mara moja Zakayo akashuka, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa. Watu wote waliokuwepo, wakaanza kunung’unika, “Amekwenda kuwa mgeni nyumbani kwa mwenye dhambi!”

Lakini Zakayo akasimama akamwambia Bwana, “Sikia Bwana, nusu ya mali yangu ninaitoa hivi sasa niwagawie maskini, na kama nimemdhulumu mtu ye yote, nitamrudishia mara nne zaidi.”

Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumba hii, kwa sababu huyu naye ni mtoto wa Ibrahimu. Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nimekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”

Hapa kuna mahubiri katika Kihispania ya Rev. D. Enric RIBAS i Baciana

******

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.