Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Matayo 25,31-46: Yesu...: "Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake pamoja na malaika wote, ataketi katika kiti chake cha utukufu cha enzi. Watu wa mataifa yote watakusanyika mbele yake, naye atawaten ganisha kama mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi. Atawaweka kondoo upande wa kulia na mbuzi upande wa kushoto. Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wa kulia, ‘Njooni ninyi mliobarikiwa na Baba yangu, urithini Ufalme mlioandaliwa tangu mwanzo wa dunia. Kwa maana nilikuwa na njaa mkanipa chakula; nilikuwa na kiu mkanipa kitu cha kunywa; nilikuwa mgeni mkanikaribisha; nilikuwa sina nguo, mkanivisha; nilikuwa mgonjwa mkaja kunitazama; na nilikuwa kifungoni mkaja kunitembe lea.’

 Kisha wale wenye haki watamjibu, ‘Bwana, ni lini tuli kuona na njaa tukakulisha au ukiwa na kiu tukakupa kitu cha kunywa ? Na ni lini tulikuona ukiwa mgeni tukakukaribisha au ukihitaji nguo tukakuvisha?  Na ni lini tulikuona ukiwa mgonjwa au ukiwa kifungoni tukakutembelea?’

 Mfalme atajibu, ‘Ninawaambia kweli, kwa jinsi ambavyo mlivyomfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, mlini fanyia mimi.’

 Kisha atawaambia wale walio kushoto kwake, ‘Ondokeni kwangu ninyi mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele alioan daliwa shetani na malaika zake.  Kwa maana nilikuwa na njaa hamkunipa chakula; nilikuwa na kiu na hamkunipa kitu cha kunywa; nilikuwa mgeni wala hamkunikaribisha; nilikuwa uchi hamkuni vika; na nilikuwa mgonjwa na gerezani nanyi hamkuja kunitazama.’

Ndipo wao pia watajibu, ‘Bwana ni lini tulikuona ukiwa na njaa au kiu, au ukiwa mgeni au ukihitaji nguo, au ukiwa mgonjwa na kifungoni na hatukukuhudumia?’

Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kwa jinsi ambavyo hamkumfanyia mmojawapo wa hawa ndugu zangu walio wadogo, hamkuni fanyia mimi.’

Basi hawa wataingia katika adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Katharina Dang

******

Mahubiri ya Johana 8,3-11:  Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya watu wote. Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Katika sheria, Musa ametuamuru kuwapiga mawe wanawake waliokamatwa wakizini, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?” 

Walim wuliza hivi kwa kumtega, kusudi wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini akaanza kuandika kwa kidole chake mavumbini. Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Asiyekuwa na dhambi kati yenu awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

 Akainama tena akaendelea kuandika chini. Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, akianza mkubwa wao. Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama pale walipomwacha.  Yesu akasimama akamwuliza, “Mama, wale waliokuwa wanakush taki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?”

Yule mwa namke akajibu, “Hakuna Bwana.”

Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Konrad Raiser

 

******

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.