TITLE: "TUNAPOHITAJI MSAADA WA MUNGU; MAKOSA MAWILI YANAYOREKEBISHIKA" - ya

 YOHANA 4:46-54 

Maneno muhimu:   Tukilinganisha miujiza; ilihusisha uaminifu;  kiongozi mkubwa katika Capernaum; -  alijishusha sana; aliamini kwamba muujiza utatokea tu ikiwa Yesu yupo hapo; tunapaswa kuamini uweza wa Yesu hata kama tusipomuona kwa macho yetu eneo la tukio lakini tunahitaji kuamini tu; aliamini ambacho Yesu alisema na akapokea wakati huo huo; "Tuamini kwamba tujapopitia mapito magumu,yeye anatuona, anataka kuwa karibu pamoja nasi."

******

Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya  Matayo 9,1-8: Yesu akaingia katika mashua akavuka ziwa, akafika katika mji wa kwao. Watu wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye kitanda chake. Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mtu ali yepooza, “Mwanangu, jipe moyo; dhambi zako zimesamehewa.” Baadhi ya walimu wa sheria wakawaza moyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” Lakini Yesu alifahamu mawazo yao. Akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? Kwani ni lipi lililo rahisi: kusema ‘Dhambi zako zimesamehewa Lakini, nitawathibitishia kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepo oza, “Simama, chukua kitanda chako uende nyumbani.” Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani. Watu walipoyaona haya, wakaogopa, wakamtukuza Mungu ambaye alitoa uwezo wa jinsi hii kwa wanadamu.

Hapa kuna mahubiri katika Kihungaria ya Czeri Kálmán

******

ya Marko 2,17: Yesu aliposikia haya aka waambia, “Wenye afya nzuri hawahitaji daktari, bali wagonjwa wanamhitaji. Sikuja kuwaalika wenye haki, bali wenye dhambi.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Katharina Dang

******

Marko 7,24-30Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia nyumba moja, ambapo hakupenda mtu afahamu yupo. Lakini hakuweza kujificha. Mama mmoja ambaye binti yake mdogo ali kuwa na pepo mchafu aliposikia habari za Yesu, alikuja mara moja akajiangusha miguuni pake. Huyo mama hakuwa Myahudi, alikuwa Mgiriki aliyezaliwa Siria-Foinike. Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu.

Yesu akamwambia, “Tuwaache watoto wale washibe kwanza, kwa maana si halali kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

Yule mama akajibu, “Ni kweli Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.”  Yesu akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, unaweza kwenda nyumbani. Yule pepo ameshamtoka binti yako.”

 Akaenda nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo amemtoka.

Hapa kuna mahubiri katika Kihispania ya Rev. D. Enric CASES i Martín

*****

Yohana 9,1-7: Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa.  Wanafunzi wake wakamwuliza, “Bwana, ni nani aliyet enda dhambi ya kusababisha mtu huyu azaliwe kipofu, ni yeye au wazazi wake?”

Yesu akawajibu, “Huyu hakuzaliwa kipofu kwa sababu yeye au wazazi wake walitenda dhambi. Jambo hili lilitokea ili nguvu za Mungu zionekane zikifanya kazi katika maisha yake. Yatupasa tutende kazi yake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana kwa maana usiku unakuja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. Wakati nipo ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.”

Baada ya kusema haya, akatema mate kwenye udongo aka tengeneza tope kwa mate yake akampaka yule kipofu machoni. Kisha akamwambia, “Nenda kanawe uso katika kijito cha Siloamu.” Neno ‘Siloamu’ maana yake ni ‘aliyetumwa.’ Yule kipofu akaenda akanawa na akarudi akiwa anaona!...

Hapa kuna mahubiri katika  Kijerumani ya Luping Huang

******

 

Mahubiri zaidi juu mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.