Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Matayo 9,27-31:  Yesu alipoondoka pale, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele kwa nguvu, “Mwana wa Daudi, tuhurumie.” 

Alipoingia ndani wale vipofu walimfuata. Akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kuwafanya muone?”
Wakamjibu, “Ndio Bwana.”
 

Ndipo Yesu akagusa macho yao akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyo amini.”

Macho yao yakafunguka. Naye akawaonya, “Angalieni mtu ye yote asijue jambo hili.”

Lakini wao walipoondoka walieneza sifa zake katika ile wilaya yote.

Hapa kuna mahubiri katika Kiingereza ya Fr. Josep Mª MASSANA i Mola OFM

 

******

Mahubiri ya Matayo 12,35-37:  Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutokana na hazina ya wema uliohifadhiwa ndani yake; na mtu mwovu hutoa yaliyo maovu kutokana na hazina ya uovu uliohifadhiwa ndani yake. “Nawaambia hakika, siku ya hukumu watu watatakiwa kujieleza kuhusu kila neno lisilo la maana walilolisema. Kwa maana kutokana na maneno yako utahesabiwa haki, na kutokana na maneno yako utahukumiwa.”

Hapa kuna mahubiri katika Kiingereza ya P. Josep LAPLANA OSB Monje de Montserrat

 

******

Mahubiri ya Matyo 15,21-28:  Na Yesu akaondoka mahali hapo akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu hizo akaja kwake, akamlilia, akasema, “Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa na pepo na anasumbuka sana.”

Lakini Yesu hakumjibu neno. Basi wanafunzi wake wakamwendea wakamwomba, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele. ”

Akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli wal iopotea.”

Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Yesu akasema, “Bwana, nisaidie!”

Yesu akajibu, “Si haki kuchu kua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

Yule mwanamke akajibu, “Ndio, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoan guka kutoka kwenye meza za mabwana wao.”

Ndipo Yesu akamwambia, “Mama, imani yako ni kubwa! Na ufanyiwe kama unavyotaka.” Tangu wakati huo mtoto wake akapona.

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Katharina Dang

******

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.