Mahubiri kwa lugha zingine:
Mahubiri ya Marko 4,26-34: Akawaambia tena, “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. Akishazipanda, usiku hulala na mchana huamka, wakati huo mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua inakuaje. Udongo wenyewe huwezesha mimea hiyo kuchipua, kukua na kukomaa. Mavuno yanapokuwa tayari, bila kupoteza wakati, yule mkulima huleta mtu akaikata hiyo mimea kwa kuwa wakati wa kuvuna umefika.”
Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuuelezea? Tunaweza kuufa nanisha na punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini. Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wakaweza kujenga viota kwenye kiv uli chake.”
Yesu alitumia mifano mingine mingi kama hii kuwaelezea neno la Mungu, kwa kadiri walivyoweza kuelewa. Hakuwafundisha lo lote kuhusu Ufalme wa Mungu pasipo kutumia mifano. Lakini ali pokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu.
Hapa kuna mahubiri katika Kiingereza ya Fr. Faust BAILO
*******
Mahubiri ya Luka 9, 51-62: Siku zake za kurudi mbinguni zilipokaribia, Yesu aliamua kwamba lazima aende Yerusalemu na akaanza safari kuelekea huko. Akatuma watu wamtangulie, nao wakaenda katika kijiji kimoja cha Samaria kumwandalia kila kitu. Lakini watu wa kijiji hicho walikataa kumpokea kwa sababu ilikuwa dhahiri kwamba ali kuwa anakwenda Yerusalemu. Basi wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, wakasema: “Bwana, unataka tuamuru moto kutoka mbinguni uwaangamize?”
Yesu akageuka, akawakemea. Wakaenda kijiji kingine. Walipokuwa wakienda, mtu mmoja akamwambia Yesu, “Nitakufu ata po pote utakapokwenda.”
Yesu akamwambia, “Mbweha wanaishi kwenye mapango yao na ndege kwenye viota vyao lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulala na kupumzika.”
Yesu alimwambia mtu mwingine, “Nifuate.”
Mtu huyo akamjibu, “Bwana, niache kwanza nikamzike baba yangu.”
Yesu akamwam bia, “Waache wafu wawazike wafu wao. Bali wewe nenda ukautan gaze Ufalme wa Mungu.”
Mtu mwingine akamwambia, “Bwana nitakufuata lakini naomba kwanza nikaage jamaa yangu.”
Yesu akamwambia, “Mtu ye yote ashikaye jembe kuanza kulima kisha akawa anageuka kutazama nyuma, hafai kwa Ufalme wa Mungu.”
Yesu Awatuma Wafuasi Sabini na Wawili
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Joaquim Nunes
*******
Mahubiri ya Yohana 6,1-15: Baadaye, Yesu alivuka hadi ng’ambo ya pili ya ziwa la Gali laya, ambalo pia huitwa bahari ya Tiberia. Watu wengi walikuwa wakimfuata kwa sababu walikuwa wamemwona akiponya wagonjwa kwa njia za ajabu. Yesu alikwenda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, ilikuwa imekaribia.Yesu alipotazama aliona umati mkubwa wa watu wanamfuata. Akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ya kuwalisha watu hawa?”
Alisema hivi kumjaribu Filipo maana yeye mwenyewe ali jua atakalofanya.Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, hazitoshi kununua mikate ya kuwapatia watu hawa japo kila mtu apate kipande kidogo.”
Mmoja wa wanafunzi wake, aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema, “Kuna mvulana mmoja ana mikate mitano na samaki wawili. Lakini hivi vitafaa nini kwa umati wote huu?”
Yesu akasema, “Waketisheni watu chini.”
Zilikuwapo nyasi nyingi mahali hapo, kwa hiyo watu wapatao elfu tano wal iweza kukaa chini. Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu, akawagawia wale watu waliokuwa wamekaa. Akawagawia pia na hao samaki wawili, kila mtu kiasi alichotaka. Watu wote wali pokwisha kula kiasi cha kutosha, aliwaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vipande vilivyobaki, kisipotee kipande cho chote.”
Basi wakakusanya vipande vya ile mikate mitano, wakajaza vikapu kumi na viwili. Watu walipoona muujiza huu alioufanya Yesu, wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii tuliyekuwa tukimtazamia!”
Yesu, akijua kwamba walitaka kumlazimisha awe mfalme wao, aliondoka hapo, akaenda milimani peke yake.
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Marc Struckmann
*******
Maubiri ya Yohana 12, 21-24: Hawa walimjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.”
Filipo akaenda akamweleza Andrea, na wote wawili wakamwambia Yesu. Yesu akawaambia, “Wakati umefika wa mimi Mwana wa Adamu kutukuzwa. Ninawaha kikishia kuwa, mbegu ya ngano isipopandwa ardhini na kufa, huba kia peke yake. Lakini ikifa inazaa nafaka kwa wingi."
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Luping Huang
*******
Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.