ALIYE MKUBWA KATIKA UFALME WA MBINGUNI - Mahubiri ya Mch. Elia M. Mande,Chuo cha Biblia na Theologia Mwika, Moshi, 16, OKTOBA 1, 2006, ya
Maneno muhimu: Wengi huwa na tamaa ya ukuu; ...Waliowakuu kweli ni wale walio wanyenyekevu na watenda mema....Kuna baadhi ya makanisa yanakosa upendo, amani na umoja kwa sababu ya wale wachache wanaotafuta na hata kung’ang’ania katika ngazi mbalimbali za ukuu kanisani....; Bwana Yesu, “Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,...."...yatupasa kuwa wanyenyekevu kama watoto wadogo. ... Majaribu mengi ya kutuangusha dhambini yanatoka ndani mwetu. ...
**************
Mahubiri kwa lugha zingine:
Mahubiri ya Matayo 13,13.16: Hii ndio sababu nazungumza nao kwa mifano; wanata zama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawae lewi....Lakini macho yenu yame barikiwa, kwa maana yanaona, na masikio yenu yamebarikiwa kwa maana yanasikia.
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Martin Hoegger
Hapa kuna mahubiri katika Kifaransa ya Martin Hoegger
******
Mahubiri ya Luka 6,36: Yesu: ...."Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.”
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Prof. Dr. Friedrich Schweitzer
*******
Mahubiri ya Yohana 3,1-10: Kiongozi mmoja wa Wayahudi wa kundi la Mafarisayo aitwaye Nikodemo, alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunafahamu kuwa wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya miujiza hii uifanyayo, kama Mungu hayupo pamoja naye.”
Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.”
Nikodemo akasema, “Inawezekanaje mtu mzima azaliwe? Anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa mara ya pili?”
Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya pili. Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uen dako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.”
Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”
Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli na huyaelewi mambo haya?..."
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Dr. Jürgen Kaiser
*******
Mahubiri ya Yohana 6, 30-35: Wakamwambia, “Utafanya ishara gani ya muujiza, tuone ili tukuamini? Utafanya jambo gani? Baba zetu walikula mana jangwani. Kama Maandiko yanavyosema, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni wakala.”’
Yesu akawajibu, “Nawaambia kweli sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni. Baba yangu ndiye anayewapa mkate wa kweli kutoka mbinguni. Kwa maana mkate wa Mungu ni yule aliyeshuka kutoka mbinguni na ambaye anatoa uzima kwa ulimwengu.”
Wakamwambia, “Bwana, tupatie mkate huo sasa na siku zote."
Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima. Ye yote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, na ye yote aniaminiye, hataona kiu kamwe...."
Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Angelika Obert
*******
Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.