Mwanzoni mwa mwezi Machi 2021, tovuti hii ilianza kufanya kazi. Kwa kutafuta fundisho kwenye mtandao, ambayo kiunganishi chake kinapaswa kuwekwa kutoka kwa maneno muhimu ya mwandishi husika. Pamoja na hayo, ingehitaji kuonyeshwa kwa maneno machache kile ambacho mtu anaweza kujifunza haswa kutoka kwa Yesu na kile kinachofanya fundisho hilo liwe na thamani sana kusomwa au kusikilizwa. Kwa kuongezea tuu, mwandishi wa fundisho husika anapaswa kuulizwa ikiwa anakubaliana na kiunganishi cha fundisho lake kutumika.

 

Kama mchungaji mstaafu, bado ninakabiliwa na shughuli nyingi peke yangu, lakini tayari nimeshashirikisha duru mbalimbali na jumuiya kadhaa za Kikristo hapa Berlin-Marzahn na kwingineko kuhusu mradi huu na nimatumaini yangu kwamba ikiwa nuru itaonekana sasa katika mradi huu itatoa fursa ya watenda kazi na wasaidizi wengine kuja hivi karibuni nakushiriki katika mradi huu.

 

Mtu yeyote anaweza kushiriki kwenye tovuti hii, kwa kufanya yafuatayo:-

- kwa kunitumia dondoo/kiunganishi kuhusu mahubiri ambayo kimsingi yanafaa hasa kwa madhumuni ya tovuti hii,

Fundisho lazima liwe limefasiriwa kutoka katika injili nne za Biblia.

Lengo la fundisho lake lazima liwe lenye kumtafakari Yesu na maneno yake.

Fundisho lake lazima liwe wazi, lazima ajiuize Je! fundisho hili limaana gani kwa Maisha yangu binafsi siku ya leo.

Fundisho lake lazima liwe mbali na kusifia, kukosoa au hata kuhukumu dhehebu/ kanisa/ kutaniko la aina yeyote ile.

• macho na masikio ya msomaji/msikilizaji yanakuwa yamelekezwa mahususi kwenye maisha yao wenyewe.

 

Kuendeleza ushirikiano zaidi inawezekana, kwa mfano:-

- kwa kunipa dondoo mbalimbali kuhusu makosa ya kiuandishi au ya kisarufi au hata kuhusu namna bora inayofaa zaidi kujieleza.

- kwa kunijulisha kuhusu matukio na mipango inayomuelezea Kristo itakayofanyika katika miaka ya 2030 – 2033.

- kwa kuifanya tovuti hii ijulikane na kupendekezwa zaidi.

- kwa kubuni tovuti hii katika lugha tofauti chini ya mwelekeo wetu na kujenga mtandao tofauti kwa ajili yake. Muundaji wa ukurasa huu alitoa maagizo kwa hili. Kwa kusudi hili, ukurasa huu umeundwa kwa urahisi kwa kadiri ilivyowezekana.

- Wakristo wa mataifa mengine au wenye ujuzi mzuri wa lugha ya ziada wanaombwa kushiriki katika kubuni na kuwajibika kwa tovuti hii.

- kwa kutafsiri maandishi kutoka kwenye tovuti hii kwa lugha nyingine, kutaruhusu kufanyika kwa kazi ya maandalizi ya tovuti za baadaye ambayo tayari imeanza kufanywa.

 

Kwa kutarajia ushirikiano wako na miaka 11 ijayo ya kutengeneza mtandao huu wa watu duniani kote wanaotaka kuheshimu na kujifunza kutoka kwa Yesu,

Katharina Dang kutoka Berlin-Marzahn.