Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya  Matayo 18,20:"Kwa maana wanapokutana watu wawili au watatu katika jina langu, hapo mimi nipo pamoja nao.”

Hapa kuna mahubiri katika Kifaransa ya Martin Hoegger (Uswisi)

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Martin Hoegger  (Uswisi)

******

 Mahubiri ya Matayo 28,1-10: Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ile ya Jumapili, Mari amu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikwenda kuliangalia kaburi. Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu Malaika wa Bwana alikuja kutoka mbinguni akalisogeza lile jiwe, akalikalia. Malaika huyo alifanana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji. Wale walinzi wa kaburi walipomwona walitetemeka kwa hofu, wakawa kama wamekufa.
 Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope. Ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. Hayupo hapa. Amefu fuka kama alivyosema. Njooni muone pale alipokuwa amelazwa. Kisha nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake hivi, amefufuka kutoka kwa wafu naye amewatangulia kwenda Galilaya, mtamwona huko. Sasa nimekwisha waambia.”
Wakiwa wamejawa na hofu na furaha nyingi, wale wanawake waliondoka upesi pale kaburini, wakaenda mbio kuwaeleza wanafunzi habari hizo.

Mara, Yesu akawatokea, akawasalimia, “Salamu!” Wale wana wake wakamwendea wakajitupa chini wakaishika miguu yake, wakam wabudu. Ndipo Yesu akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, wataniona huko.”

Hapa kuna mahubiri katika Kifaransa ya Martin Hoegger (Uswisi)

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Martin Hoegger (Uswisi)

******

Mahubiri ya Luka 24,13-15: Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, nao walikuwa wakizungumzia mambo yote yaliyotokea.  Wali pokuwa wakizungumza, Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao,  lakini wao hawakumtambua.  Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumzia wakati mnatembea?” Wakasimama , nyuso zao zikionyesha huzuni.  Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamwambia, “Nadhani ni wewe tu katika watu wote wanaoishi Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotokea siku hizi chache zilizopita.”

Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu “Mambo yaliyompata Yesu Mnazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Makuhani wakuu na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa na wakamsulubisha. Na sisi tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angeliikomboa Israeli. Zaidi ya hayo leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtua; walikwenda kaburini leo alfajiri  lakini hawakuukuta mwili wake. Waliporudi walisema wamewaona malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai. Baadhi yetu walikwenda kaburini wakakuta mambo ni kama walivyoelezea wale wanawake, ila yeye mwenyewe hawakumwona.”

 Kisha Yesu akawaambia, “Ninyi ni watu wajinga. Mbona mnaona ugumu kuamini mambo yote yaliyosemwa na Manabii?  Je, haikumpasa Kristo kuteswa na kwa njia hiyo aingie katika utukufu wake?”

Akawafafanulia maandiko yalivyosema kumhusu yeye, akianzia na maandiko ya Musa na kupitia maandiko yote ya manabii.

Walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea na safari.  Lakini wakamsihi akae nao wakisema, “Kaa hapa nasi kwa maana sasa ni jioni na usiku unain gia.”

Basi akaingia ndani kukaa nao.  Alipokuwa nao mezani, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia.  Ndipo macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua! Lakini akatoweka, hawakumwona tena.

Wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuchangamka kwa furaha alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?”

Wakaondoka mara moja, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusany ika wakisema, “Ni kweli Bwana amefufuka! Amemtokea Simoni.”

Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotokea njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake.

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Luping Huang

******

Yohana 21, 1-14: Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: Simoni Petro, Tomaso aitwaye Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.”

Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.”

Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote. Kulipopambazuka, Yesu alisimama ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua. Yesu akawaambia, “Wanangu, mmepata samaki wo wote?”

Wakamjibu, “La.”

Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.”

Walivyofa nya hivyo walipata samaki wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika mashua! Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!”

Petro aliposikia haya akajifunga nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi.  Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate.  Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua.” 

Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. Yesu akawaambia, “Njooni mle.”

Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?”

Walijua hakika ya kuwa ni Bwana.  Yesu akaenda akachu kua ile mikate na baadaye samaki, akawagawia. Hii ilikuwa ni mara ya tatu Yesu kujitambulisha kwa wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Dr. Petra Zimmermann

*****

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.