“IWENI NA HURUMA KAMA BABA YENU WA MBINGUNI” - Mahubiri ya DAWSON CHAO, 20, OKTOBA 29, 2006, ya

 LUKA 6:27 – 38 

 

Maneno muhimu: Kuna msemo wa Kiswahili ...; Wapendeni adui zenu; - Hili ni jambo gumu peke yetu pasipo msaada wa kimungu hatuwezi....;  Jirani yangu mmoja ametamani sehemu ndogo ya shamba langu...; ...akiri pia kwamba mimi siyo mkamilifu.... Tusidharauliane na kukukumiana, tumwangalie Kristo; tujihadhari tusiwakwaze wenzetu hata kama ni wa imani tofauti.

 

 

***************

Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Matayo 5,38-48: Yesu: ...“Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini mtu akikupiga kwenye shavu la kulia, mgeuzie na shavu la kushoto pia;  na kama mtu akitaka kukushtaki achukue shati lako, mwachie achukue na koti pia. Na kama mtu akikulazimisha uende kilometa moja naye, fanya zaidi, nenda naye kilometa mbili. Mtu akikuomba kitu mpe, na usikatae kumsaidia mtu anayetaka kukukopa. “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Umpende jirani yako na umchukie adui yako.’ Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa,ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaanga zia jua lake watu waovu na watu wema; na pia huleta mvua kwa wenye haki na wasio haki. Kama mkiwapenda wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Hata wenye dhambi hufanyiana hivyo. Na kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, mnafanya nini zaidi ya wengine? Hata watu wa mataifa wasiomjua Mungu, hufanya hivyo.  Kwa hiyo inawapasa ninyi muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Katharina Dang

Hapa kwa toleo la Kivietinamu

******

Mahubiri ya Matayo 26,47- 56:  Alipokuwa anazungumza, Yuda, mmojawapo wa wale kumi na wawili, akafika,akifuatana na umati wa watu wenye mapanga na mar ungu. Walikuwa wametumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu.

 Yuda alikuwa amepatana na hao watu kuwa, ‘Nitakayembusu ndiye, mkamateni.’ Basi alipofika, alimwendea Yesu moja kwa moja, akamsalimia, “Salaam, Rabi!” Akambusu. Yesu akamjibu, “Rafiki, umekuja kufanya nini hapa?”

Basi wale watu wakasogea, wakamkamata Yesu. Ndipo mmojawapo wa wafuasi wa Yesu ali poona hivyo, akachukua panga lake, akampiga nalo mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga. Unadhani siwezi kumwomba Baba yangu aniletee mara moja majeshi kumi na mbili ya malaika? Lakini nikifanya hivyo yatatimiaje Maandiko yale yasemayo kwamba mambo haya lazima yato kee?”

Wakati huo Yesu akawaambia ule umati, “Mmekuja kunika mata kama mnyang’anyi kwa mapanga na marungu? Mbona siku zote nilikaa Hekaluni na kufundisha lakini hamkunikamata? Lakini haya yametokea ili Maandiko ya manabii yatiimie.”

Ndipo wana funzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Fernande Enns

******

 

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.