Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Matayo 5,1-10: Yesu alipoona umati wa watu, alipanda mlimani akaketi chini. Wanafunzi wake wakamjia, naye akaanza kuwafundisha akisema:
“Wamebarikiwa walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbin guni ni wao.
Wamebarikiwa wanaoomboleza; maana watafarijiwa.
Wamebarikiwa walio wapole; maana watairithi nchi.
Wamebari kiwa wenye hamu ya kutenda haki; maana wataridhishwa.
Wamebari kiwa walio na huruma; maana nao watahurumiwa.
Wamebarikiwa walio na moyo safi; maana watamwona Mungu.
Wamebarikiwa walio wapatanishi; maana wataitwa wana wa Mungu. 
Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Dr. Wolfgang Vögele

******

Mahubiri ya Marko 1,40-45:  Akaja mtu mwenye ukoma, akapiga magoti mbele ya Yesu akamsihi, “Ukitaka, unaweza kunitakasa.” Yesu akamwonea huruma, akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka upone, takasika.”

Mara ukoma wote ukaisha akapona kabisa. Yesu akamruhusu aende lakini akamwonya, “Usimwambie mtu ye yote habari hizi; bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka ya utakaso kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwa watu.”

 Lakini yule mtu alikwenda akatangaza habari za kuponywa kwake kila mahali. Kwa hiyo Yesu hakuweza tena kuingia katika vijiji na miji waziwazi isipokuwa alikaa sehemu zisizo na watu, nao wakamfuata huko kutoka pande zote.

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Tim Schlotmann

*****

Mahubiri ya Luca 5, 27-32:  Baada ya haya Yesu alimwona afisa mmoja mtoza kodi jina lake Lawi akiwa ofisini mwake, akamwambia, “Njoo uwe mmoja wa wanafunzi wangu.”
Lawi akaacha vyote, akaondoka, akamfuata Yesu. Baadaye Lawi akafanya karamu kubwa kumkaribisha Yesu nyumbani kwake. Watoza kodi wengi walikuwa miongoni mwa watu wal ioalikwa. Basi baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria ambao walikuwa kundi moja wakawalalamikia wanafunzi wa Yesu wakisema, “Mbona mnakula na kunywa na wenye dhambi?” '
Yesu akawajibu, “Wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. Sikuja kwa ajili ya wenye haki bali nimekuja kuwaita wenye dhambi ili watubu.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Rev. D. Joan Carles MONTSERRAT i Pulido

 

******

 

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.