Mahubiri kwa lugha zingine:

Matayo 21,1-11: Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, aka waagiza, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu na mkiingia mtamwona punda amefungwa na mwanapunda pamoja naye. Wafungueni mniletee. Kama mtu akiwauliza lo lote, mwambieni, ‘Bwana anawa hitaji."
Haya yalitokea ili kutimiza utabiri wa nabii aliposema,  ‘Mwambieni binti Sayuni, tazama mfalme wako anakuja kwako ni mnyenyekevu, na amepanda punda, mwanapunda, mtoto wa punda.’

Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyowaagiza. Wakamleta yule punda na mwanapunda. Wakatandika mavazi yao juu ya hao punda na Yesu akaketi juu yake. Umati mkubwa wa watu wakatandika nguo zao barabarani, wengine wakakata matawi ya miti wakayatandaza barabarani. Ule umati wa watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapiga kelele wakisema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi . Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana! Hosana juu mbin guni.”

Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukajawa na hekaheka, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” 

Ule umati wa watu wakajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Meike Waechter

******

Yohana 7,37-39: " Siku ya mwisho ya sikukuu, ambayo kwa kawaida ndio ili kuwa kilele cha sherehe, Yesu alisimama akasema kwa sauti kuu, “Mtu ye yote mwenye kiu na aje kwangu anywe. 38 Kama Maandiko yasemavyo, ye yote aniaminiye, vijito vya maji yaletayo uzima vitatiririka kutoka moyoni mwake.” 39 Yesu alisema haya kuhusu Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini Yesu wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa bado hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajainuliwa na kutukuzwa."

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Dr. Werner Schmückle

******

Yohana 11, 1.3.17-27.38b-46.53: Palikuwa na mtu mmoja jina lake Lazaro ambaye aliugua. Yeye aliishi katika kijiji cha Bethania pamoja na dada zake wawili, Mariamu na Martha. ... Hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa sana.” ...

Yesu alipowasili alikuta Lazaro alikwisha zikwa siku nne zilizopita. Kwa kuwa kijiji cha Bethania kilikuwa umbali wa kama kilometa tatu tu kutoka Yerusalemu, Wayahudi wengi wal ikuwa wametoka mjini kuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa kifo cha ndugu yao. Martha aliposikia Yesu amefika, alitoka kwenda kumpokea, ila Mariamu akabaki amekaa ndani.  Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangali kufa. Na hata sasa ninafahamu kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakutimizia.” 

Yesu akamwambia, “Kaka yako atakuwa hai tena.” 

Martha akamjibu, “Ndio, ninajua ya kuwa atakuwa hai tena wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” 

Yesu akamwambia, “Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi; na ye yote anayeishi akiwa ananiamini hatakufa kamwe. Je, unaamini haya?”

Martha akajibu, “Ndio Bwana; ninaamini ya kuwa wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye ange kuja ulimwenguni.” ...

Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa kwa jiwe. Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.”

Dada yake mare hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu azikwe.”

Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?” 

Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia. Ninajua ya kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa, ili wapate kuamini ya kuwa umenituma.”

Baada ya kusema haya akapaaza sauti akaita, “Lazaro, toka nje!”

Yule aliyekuwa amekufa akatoka, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa. Yesu akawaambia, “Mfungueni awe huru!” 

Wayahudi wengi waliokuja kumfariji Mariamu, walipoona yaliyotokea wakamwamini Yesu.  Lakini wengine walikwenda kwa Mafarisayo wakawaambia mambo Yesu aliyofanya....Tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi wakawa wanafanya mipango ili wamwue Yesu.

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Prof. Dr. Dorothea Wendebourg

******

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.