Mahubiri kwa lugha zingine:

Mahubiri ya Luka 23,33-49: Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,” wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.

Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. Watu wakasi mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.”

Askari nao wakam wendea, wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe, wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”

Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake: “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.”

Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”

Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.”

Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.”

Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”

Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa,  kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili.  Yesu akapaza sauti akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.”

Baada ya kusema haya, akakata roho.

Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.”

Na watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hilo walipoy aona hayo, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.

Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wanawake wal iokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyata zama mambo haya. Yesu Azikwa Kaburini

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani ya Katharina Dang

 

*******

Mahubiri ya Yohana 8,1-11: Lakini Yesu akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni. Alfajiri Yesu akaja tena Hekaluni, watu wengi wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha.  Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya watu wote. Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Katika sheria, Musa ametuamuru kuwapiga mawe wanawake waliokamatwa wakizini, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?”

Walim wuliza hivi kwa kumtega, kusudi wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini akaanza kuandika kwa kidole chake mavumbini. Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Asiyekuwa na dhambi kati yenu awe wa kwanza kumtupia jiwe.”

Akainama tena akaendelea kuandika chini. Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, akianza mkubwa wao. Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama pale walipomwacha. Yesu akasimama akamwuliza, “Mama, wale waliokuwa wanakush taki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?”

Yule mwa namke akajibu, “Hakuna Bwana.”

Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”

Hapa kuna mahubiri katika Kijerumani  ya Joaquim Nunes

Hapa kuna mahubiri katika Kireno ya Joaquim Nunes

 

******

Mahubiri juu ya mada yataunganishwa hapa hivi karibuni.